Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha
Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, mwili wako unahitaji virutubishi ili kusaidia ukuaji wa mwili, kama ni kijana mwili wako una mahitaji maalumu unayoyahitajia kudhamini makuzi ya kiafya ya mwili wako wakati wa utu uzima na wakati unapokuwa mtu mzima unahitaji kuwa na uzito uliolingana na mwili wa wastani. Tukiangalia katika upande wa Akina mama wajawazito na wale wanaonyonyesha nao pia wana vyakula vyao maalumu wanavyohitajia tofauti kabisa na wanawake wengine. Uchunguzi wa kitiba uliofanywa unaonyesha kuwa, hali ya kiafya ya mama mjazito huwa na athari mbalimbali kwa mtoto atakayezaliwa. Vile vile kuna ushahidi mkubwa kuwa magonjwa sugu ya watu wazima huanzia wakati mtoto bado akiwa tumboni mwa mama yake akiwa katika hali ya kiluilui au (foetus). Kwa hivyo akina mama wajawazito wanashauriwa kuzingatia vyakula wanavyokula kabla na baada ya kushika mimba. Sasa tuangalie athari za chakula kwa...