UVUMILIVU (SUBRA) NI NGUZO KUBWA YA MAFANIKIO

 Uvumilivu ni nguzo ya mafanikio kwani kila jambo la kheri lina vikwazo ,Naomba usome kisa kifupi hiki ufaidike na wewe   (Kijana mmoja alipata nafasi ya kimasomo katika nchi fulani ya kigeni bure kila kitu atalipiwa na shule yeye alitakiwa kuripoti tu nakuanza masomo ilipo fika tarehe yakuripoti shule alitakiwa kufika uwanja wandege saa saba kamili mchana (01:00) kwaajiri ya kuanza safari yake alifurahi sana alihisi ni kama ndoto kwake kwani siku zote alipenda aipate nafasi hiyo lakini aliikosa hivyo aliwaaga marafiki zake huku akiwa katika furaha kubwa machozi yakimdondoka kwa furaha aliyo nayo lakini alipo fika uwanja wa ndege alichelewa dakika 15 hivyo safari yake ikasitishwa hato safiri tena pia zile ofa zote za kimasomo alizo pewa ziliishia palepale inauma sana kijana aliumia sana akalia pia alizungumza maneno mabaya sana alishindwa kuvumilia alifikia hadi kumkufuru alie muumba ilibidi arudi  nyumbani alikua katika huzuni kubwa sana alipo fika nyumba alijifungia ndani alikaa muda mrefu sana ndani nje anajiskia aibu kutoka maana watu wengi alisha waaga hivyo akaamua kuwasha TV ili muda uende kidogo lakini lakusikitisha zaidi alipo tazama katika TV taarifa ya habari ilikua ikitolewa nakatika taarifa hiyo ilikua inazungumzia ajari kubwa ya ndege iliyo ondoka saa saba kamili ( 01:00 ) kuwa imeripuka na watu wote wamefariki dunia.    Watukufu waislamu mtume (sw) anasema (niajabu ilioje katika mambo ya muumin kwahakika mambo yake yote kwake nikheri anapo pata jambo la kumfurahisha humshukuru Allah basi kwakufanya hivyo inakua kheri kwake na anapopatwa najambo baya la kumdhuru anavumilia basi nakwakufanya hivyo inakua nikheri kwake) watukufu waislamu tunatakiwa tufahamu kua anae simamia maisha yetu ni Allah hivyo ilitufanikiwe ni lazima tufate muongozo wake alio tuwekea kwani unaweze kupenda kitu huenda kikawa na madhra na wewe pia waweza chukia kitu kumbe kina kheri na wewe sasa nini chakufanya ni

kufanyia kazi maneno haya matukufu ya mtume  (sw) kua mvumilivu(subra)

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

kaburi la mtume YUSHA

STAHA NA HAYA KWA MWANAMKE